MASHARTI YA MATUMIZI YA KITASA
Toleo: 1.0 · Tarehe: 02/10/2026
- Kuhusu huduma. Kitasa ni jukwaa la WesanDev la kuhifadhi kumbukumbu za upangaji (kodi, risiti, mikataba, bili za pamoja, umeme) na soko la matangazo ya nyumba, viwanja, madalali na vifaa vya ujenzi. Kwa sasa huduma ni bure.
- Akaunti. Unatumia namba ya simu yako halali. Unawajibika kwa matumizi yote ya akaunti yako. Usimpe mtu namba ya OTP.
- Kitasa haishiki pesa. Malipo hufanyika nje ya Kitasa (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, benki, taslimu n.k.). Kitasa inarekodi tu malipo hayo. Hatuhusiki na fedha zilizotumwa kwa mtu asiye sahihi.
- Risiti na uthibitisho. Malipo yanakuwa "yamethibitishwa" pale mwenye nyumba au msimamizi anapoyathibitisha. Picha za ushahidi ni za kusaidia tu. Risiti iliyotolewa haiwezi kubadilishwa; makosa hurekebishwa kwa risiti ya marekebisho. Unakubali kwamba kumbukumbu hizi zinaweza kutumika kama ushahidi kati ya pande mbili.
- Mikataba. Kiolezo cha mkataba ni msaada tu na si ushauri wa kisheria. Pande zote zinawajibika kukisoma na kukirekebisha. Kukubali kupitia OTP ni ishara yako ya kukubali maandishi ya mkataba.
- Bili za pamoja. Wanachama wa nyumba wataona majina yako, kiasi chako na hali ya malipo ya bili za pamoja. Kodi yako haionyeshwi kwenye ubao.
- LUKU. Makadirio ya umeme ni ya kukisia kulingana na taarifa mnazoweka; si taarifa rasmi za TANESCO.
- Soko. Matangazo yote hukaguliwa kabla ya kuonekana. "Imeidhinishwa" inamaanisha tumelikagua tangazo; "Muuzaji aliyethibitishwa" inamaanisha tumethibitisha utambulisho wa muuzaji. Hatuthibitishi umiliki wa mali wala ubora wa bidhaa. Usilipe kabla ya kuona mali/bidhaa na nyaraka zake. Kitasa si sehemu ya makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji.
- Yasiyoruhusiwa. Matangazo ya uongo, utapeli, bei za kudanganya, maudhui ya matusi au yasiyofaa, kutumia namba ya mtu mwingine, kuweka taarifa za mtu bila ridhaa yake, kujaribu kuvunja usalama wa mfumo.
- Kusimamisha akaunti. Tunaweza kuondoa matangazo au kusimamisha akaunti zinazokiuka masharti haya. Kumbukumbu za kifedha zitabaki kwa ajili ya pande nyingine.
- Ukomo wa dhima. Huduma inatolewa "kama ilivyo". Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, WesanDev haiwajibiki kwa hasara zinazotokana na makubaliano kati ya watumiaji, matangazo ya watumiaji, au kukatika kwa huduma.
- Faragha. Angalia Sera ya Faragha.
- Mabadiliko. Tunaweza kubadilisha masharti haya; tutakujulisha ndani ya app.
- Sheria. Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Mawasiliano. support@wesandev.com.
KITASA TERMS OF SERVICE (English)
Version: 1.0 · Date: 02/10/2026
- The service. Kitasa, operated by WesanDev, keeps tenancy records (rent, receipts, contracts, shared bills, electricity) and runs a marketplace for housing, plots, brokers and construction materials. It is currently free.
- Accounts. Use your own valid phone number; you are responsible for activity on your account; never share your OTP.
- Kitasa does not hold money. Payments happen outside Kitasa. Kitasa only records them and is not responsible for money sent to the wrong person.
- Receipts and confirmation. A payment is "confirmed" when the landlord or caretaker confirms it. Evidence images are supporting only. Issued receipts cannot be changed; mistakes are fixed with a correction receipt. You agree these records may be used as evidence between the parties.
- Contracts. The contract template is a convenience, not legal advice. Accepting by OTP signifies your agreement to the contract text.
- Shared bills. House members see your name, share and payment status for shared bills. Your rent is never shown on the board.
- LUKU estimates are approximations based on data entered by users, not official TANESCO data.
- Marketplace. All listings are reviewed before going live. "Approved" means we reviewed the listing; "Verified seller" means we verified the seller's identity. We do not verify ownership of property or the quality of goods. Do not pay before seeing the property/goods and documents. Kitasa is not a party to deals between users.
- Prohibited: false or fraudulent listings, misleading prices, abusive content, using another person's number, posting someone's data without consent, attacking the system.
- Suspension. We may remove listings or suspend accounts that break these terms; financial records remain for the other party.
- Liability. Provided "as is"; to the extent permitted by law, WesanDev is not liable for losses from dealings between users, user listings, or service interruptions.
- Privacy. See the Privacy Policy.
- Changes. We may update these terms and will notify you in the app.
- Governing law. Laws of the United Republic of Tanzania.
- Contact. support@wesandev.com.